Waziri mkuu wa China Wen Jiabao apokelewa nchini Ujerumani katika ziara yake barani Ulaya
Imechapishwa:
Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao ameendelea na ziara yake Barani Ulaya na sasa amewasili nchini Ujerumani ambapo amekutana na Kansela Angela Merkel ambapo wanatarajiwa kuwa na mazungumzo yatakayolenga uhusiano wa kiuchumi.
Matangazo ya kibiashara
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kusaini makubaliano ya kushirikiana kiuchumi ambayo yanatajwa huenda yakawa na thamani ya mabilini ya euro lengo likiwa ni kuhakikisha wanasonga mbele kibiashara.
Waziri Mkuu Wen amewasili Ujerumani akitokea nchini Uingereza ambapo kwa pamoja na Waziri Mkuu David Cameron walikubaliana kusaini mpango wa kibiashara wenye thamani ya pauni bilioni moja.