Cyprus

Mlipuko mkubwa wasikika katika kambi ya kijeshi ya wanamaji nchini Cyprus

Milipuko ya bomu umesikika mapema asubuhi ya Jumatatu Julay 11 katika kituo cha jeshi la majini mjini Zygi katika kisiwa cha Cyprus. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu tukio hilo, lakini kituo cha radio ya taifa kinasema kati ya watu 8 na 12 wameuawa. Mlipuko huo huenda ni wa ajali. Majumba yalio karibu na kambi ya jeshi hilo na kituo kimoja cha umeme vilimeharibika. Gari za kubeba wagonjwa zilifika mapema eneo hilo, wito wa kuchangia damu umetolewa.

Timu ya waokoaji
Timu ya waokoaji RFI
Matangazo ya kibiashara

Milipuko hiyo imetokea katik akambi ya jeshi la Evangelos Florakis kaskazini mwa kisiwa hicho. Kambi hiyo ya jeshi la Cyprus ipo katika maeneo ya mji wa pwani ya Larnaca na Limassol.

Kwa mujibu wa runinga ya taifa, mlipuko mkubwa umesikika mapema asubuhi ya Jumatatu. Watu 12 ndio wameiaga dunia, huku radio ikisema kuwa ni wa tu 11. Wizara ya ulinzi haijasema lolote kuhusu idadi hiyo. Hata hivyo msemaji wa swizara amesema “ kuna idadi ya watu waliokufa na wwngine wamejeruhiwa” waathiriwa huenda ni wazima moto na wanajeshi wa ulinzi wa taifa.

Chanzo cha mlipuko huo chaweza kuwa itokea katika ghala la silaha. Polisi inasema kasha mbili za unga wa baruti ziliwaka na kusababisha mlipuko huo. Kasha hizo za silaha mali ya Irani zilikamatwa mwaka 2009 katika mashuwa mojwapo, yathibitisha radio ya taifa.

Maeneo ya karibu ya kambi hiyo pia yameguswa na milipuko hiyo majumba yaliokaribu yameharibika. Moto mkali uliosababishwa na milipuko hiyo ilitokea. Wizara ya ulinzi imesema kuwa kituo cha umeme kimeharibika, hivyo eneo kubwa la Vassilikos ililoko katibu na kituo hicho hakina umeme.