Urusi-Ajali

watu 100 wahofiwa kufa maji nchini Urusi baada kutokea tufani kubwa iliopiga boti waliokuwemo

Shuguhuli za kuwaokoa watu zapapmba moto
Shuguhuli za kuwaokoa watu zapapmba moto REUTERS/Yegor Aleev

Takriban watu mia moja wanahofiwa kufa maji huku Waokoaji wako katika mto Volga mjini Moscow nchini Urusi kuwatafuta watu zaidi ya 100 waliozama majini, baada ya boti waliokuwa wamepanda kuzama baada ya tufani kubwa kuipiga meli hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa kutoka wizara inayoshughulikia maswala ya dharura wamesema kuna matumaini madogo sana ya kuwapata watu waliozama wakiwa hai.

Abiria Waliookoka na ajali hiyo wamesema tufani iliyopiga jana jioni ilisababisha Boti kuyumba yumba kabla ya kupinduka na kuzama dakika chache baadae.

Boti hiyo ilikuwa imebeba takriban watalii 150 na zaidi ya wafanyakazi 30 wa boti hiyo ikifanya safari zake za kawaida.