Italia-Uingereza

Inter Milan yakana kupokea ombi la kutaka kumnunua Wesley Sneijder

Wesley Sneijder.
Wesley Sneijder. Reuters

Kiongozi wa kiufundi wa klabu ya Inter Milan ya Italia Marco Branca amesisItiza kuwa uongozi wa klabu hiyo haujapata ombi lolote rasmi la kutaka kumuuza kiungo wake wa kati Wesley Sneijder .

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa wa ligi ku ya soka nchini Uingereza Manchester United, wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Sneijer lakini InterMilan inasema, hakuna mazungumzo wala maafikiano ambao yamefanyika na hawana mpango wa kumuuza.

Mwezi uliopita, Sneijer alinukuliwa na mtandao wa klabu ya Inter Milan akisema kuwa anafurahia kuchezea klabu hiyo na hana mpango wa kuondoka.

Magazeti ya Uingereza yamekuwa yakichapisha habari kuwa Manchester United imetenga Pauni Milioni 35 kumsajili mchezaji huyo, msimu ujao.