FBI kuchunguza ripoti ya uharamia wa simu zikiwalenga waathiriwa wa septemba 11
Imechapishwa:
Shirika la Marekani la Ujasusi la FBI huenda likachunguza ripoti kuwa shirika la habari la Rupert Murdoch la huko Uingereza la News Corportation, lilihusika na uharamia wa habari kupitia simu zikiwalenga waathiriwa wa shambulizi la bomu la Septemba kumi na moja mwaka 2001.
Hatua hiyo inajiri kutokana na shinikizo kutoka kwa wabunge wa Republican,kama anavyoeleza Peter King mmoja wa wabunge wa Congress kutoka chama cha Republican.
Huko Uingereza, mmiliki wa shirika hilo la habari la News Corporation Rupert Murdoch na mwanawe James wamekubali kufika mbele ya wabunge wa Uingereza juma lijalo kujibu maswali kuhusu shutuma hizo.
Nick Clegg Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza amesema ni muhimu kwa Murdoch kufika mbele ya wabunge hao ili kuhojiwa.