Uturuki

Mgogoro wa Libya kujadiliwa leo mjini Istambul

Afriquinfos

Wanadiplomasia kumi na watano watakutana hii leo mjini Instambul nchini Uturuki kujadili suluhu ya kisiasa juu ya mgogoro wa Libya na namna ya kuwasaidia waasi wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utawahusisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary clinton, william Hague wa uingereza, waziri wa mambo ya nje wa ufaransa Alain Jupe na Franco Fratini wa Italia.

Mwanadiplomasia nchini Uturuki amesema Ajenda kubwa na muhimu ya mkutano huo wa leo ni kuondoka madarakani kwa amani kwa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi.

Kiongozi wa waaasi katika maswala ya mambo ya nje, Mahmood Jibril atahudhuria mkutano huo ambao wanadiplomasia watajadili maswala ya misaada ya kijeshi na fedha ambavyo vitawasilishwa kwa waasi wiki za hivi karibuni.

Serikali ya China na Urusi wamekataa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.