Uingereza

Mkurugenzi wa shirika la News Corporation Rebekah Brooks ametangaza kuachia wadhfa wake

Kufuatia wiki ya msukosuko kwa serikali ya Uingereza kuhusiana na sakata la uharamia wa taarifa kwa njia ya simu uliofanywa na gazeti la News of the world, mkurugenzi mtendaji wa shirika la News Corporation Rebekah Brooks ametangaza kuachia wadhfa huo.

Rebekah Brooks ajiuzulu
Rebekah Brooks ajiuzulu Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika barua yake aliyomtumia mmiliki wa shirika hilo Rupert Mudoc na mtoto wake james Mudoc, Brooks amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona anahitaji kuwajibika kama kiongozi wa shirika hilo na kuomba radhi kwa wananchi walioathirika na kuchapishwa kwa taarifa zao za siri.

Rebekah Brooks ambaye ameitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 22 na pia aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la the news of the world mwaka 2003 alikuwa mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo waliokuwa mstari wa mbele kutetea uamuzi wa kuchapishwa kwa taarifa za siri.

Uamuzi wake umekuja ikiwa siku chache zijazo yeye na mmiliki wa makampuni ya News Corporation Rupert Mudoc watokea mbele ya bunge la nchi hiyo kujibu tuhuma ambazo zimeikumba kampuni hiyo.

Mudoc mwenyewe amekiri kupokea barua ya Brooks na kuikubali huku akimwagia sifa kwa uchapakazi ambapo tayari wamemtangaza Tom Mockridge ambaye ni mkuu wa shirika la habari la SKY kuchukua nafasi ya Rebekah Brooks.