Norway

Mtuhumiwa wa mauaji ya Norway ataka daktari wa Japan amchunguze

REUTERS/Jon-Are Berg-Jacobsen

 Mtuhumiwa wa mashambulizi yaliyotokea nchini Norway Anders Breivik ametaka apatiwe mtaalam kutoka nchini Japan ili afanye kazi ya kuchunguza afya yake kabla ya vithibitisho hivyo kupelekwa mahakamani.

Matangazo ya kibiashara

 

 

Mwanasheria wa Breivik, Geir Lippestad amesema ombi hilo la mteja wake limekwenda sambamba na kauli ya kutaka atumie lugha ya kiingereza mahakamani wakati anajitetea kwenye shauri la mauji ya watu sabini na sita linalomkabili.

Kwa upande wao Jeshi la Polisi limeanza kufanya usafi kwenye eneo la Utoeya wakiwa na lengo la kurejesha hali kama ilivyokuwa awali baada ya madhara kutokea baada ya tukio hilo.

Mtuhumiwa huyo pia ametaka uongozi wa Serikali ya Norway na jeshi la polisi kujiuzulu kutokana na kushindwa kuwajibika inavyopswa wakati tukio hilo.

Madaktari wa Norway watakiwa kutoa ripoti yao juu ya afya ya Andres Breivik ili ijulikane kama yuko tayari kiafya kuwezesha kesi yake kuendelea kusikilizwa.

Hata hivyo mpaka sasa mtuhumiwa huyo wa mauaji hajatoa taarifa yoyote kama atatoa ushirikiano kwa mahakama ama la.