Ufaransa

Mkuu wa IMF Christine Lagarge matatani kwa ufisadi

Reuters/Shannon Stapleton

Mahakama nchini Ufaransa imeamuru ufanywe uchunguzi dhidi ya mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarge.

Matangazo ya kibiashara

 

Mahakama hiyo imeagiza uchunguzi huo ufanywe dhidi yake kutokana na tuhuma za ufisadi alipokuwa waziri wa fedha nchini humo.

Lagarde anatuhumiwa kuwa alishinikiza benki mmoja nchini humo kutoa fedha ili kufadhili kampeni za rais Nicolas Sarkozy katika uchaguzi wa rais nchini Ufaransa.

Hata hivyo Lagarde amekana kufanya kosa lolote na wachambuzi wa mambo wanahisi kuwa tuhuma hizi zinaweza kumharibia wasifu wake kama Mkurugenzi Mkuu wa IMF.