PARIS-FRANCE

Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa kushirikiana kunusuru mataifa yao na mgogoro wa kiuchumi

Kansela wa Ujerumani Angela Markel (kushoto) na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy (kulia) wakizungumza wakati wa mkutano wao wa pamoja mjini Paris, jana
Kansela wa Ujerumani Angela Markel (kushoto) na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy (kulia) wakizungumza wakati wa mkutano wao wa pamoja mjini Paris, jana REUTERS/Charles Platiau

Kansela wa Ujerumani Angela Markel na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wamekubaliana kwa kauli moja nchi zao kushirikiana katika kukabilina na mgogoro wa kiuchumi ambao unayakumba mataifa ya Ulaya na kusababisha kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Euro.

Matangazo ya kibiashara

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Paris wakati wakifanya mkutano wa pamoja, viongozi hao wameyataka mataifa yaliyoko katika umoja wa Ulaya kusimamia vizuri rasilimali zao pamoja na kutekeleza kwa wakati sera za uchumi kuinusuru sarafu ya Euro.

Kansela Markel amesema kuwa serikali yake tayari imeanza utekelezaji wa usimamizi wa sera yake ya kukuza uchumi pamoja na kusimamia taasisi za fedha nchini humo kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchumi wa taifa hilo unaendelea kupanda na kuwa katika halin nzuri.

Kwa upande wake rais Nocolas Sarkozy amesema kuwa serikali yake imeandaa mkakati maalumu wa kuongeza tozo la kodi katika taasisi za fedha ambazo zimekuwa zikichangia kiduchu katika sekta ya uchumi hatua inayolenga kuweka uwiano sawa wa ulipaji kodi kati ya taasisi za fedha na makampuni makubwa ya kibiashara.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekosolewa na wachambuzi wa masuala ya uchumi wakisema kuwa walishindwa kutoa kauli ya pamoja wakati wa mkutano wao uliotangulia kuhusu kunusuru mataifa amabyo yameingia katika mgogoro wa kifedha.