Pata taarifa kuu
UTURUKI-ISRAEL

Serikali ya Uturuki imemtimua Balozi wa Israeli huko Ankara

Reuters
Ujumbe kutoka: Nurdin Selemani Ramadhani
Dakika 2

Serikali ya Uturuki imemtimua Balozi wa Israel huko Ankara na kusitisha uhusiano wao wa kijeshi na taifa hilo baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa UN kuthibitsha nchi hiyo ilitumia nguvu kubwa kuzuia meli ya misaada iliyokuwa inaeleka Ukanda wa Gaza.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu ndiye ambaye ametangaza hatua hiyo ya kutimuliwa kwa balozi huyo na kuweka bayana anatakiwa kurejea kwao haraka iwezekanavyo baada ya kubaini nchi yake ilitumia nguvu kubwa kwenye operesheni hiyo.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Uturuki hakuishia kutangaza kutimuliwa kwa Balozi wa Israel tu bali akaweka bayana hatua yao ya kusitisha makubaliano ya kijeshi yaliyokuwa yamefikiwa baina ya nchi hizo mbili.

Davutoglu amesema nchi yake inajiandaa kukosoa kile ambacho kinaonekana ni haki kwa Israel kutekeleza uamuzi wake wa kuzuia meli iliyokuwa na wanaharakati wa Uturuki kutokwenda Ukanda wa Gaza.

Uamuzi wa serikali ya uturuki umekuja saa chache baada ya kuvuja kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa UN juu ya tukio la kushambuliwa kwa meli ya Uturuki na kusababisha vifo vya wanaharakati tisa.

Katika hatua nyingine Rais wa Uturuki Abdullah Gul amesema hawaitambui ripoti inayotarajiwa kutolewa rasmi ya UN kwani amesema haina umuhimu wowote kwa nchi yake na pia ni batili.

Rais Gul amesema hatua ambazo zimechukuliwa na nchi yake ndiyo muafaka kwani nchi ya Israel imekaidi hatua ya kuomba radhi ambayo ilipendekezwa na Uturuki na badala yake wanajiona wamefanya kitu sahihi.

Tukio la kuishambulia meli ya Mavi Marmara lililotokea mwaka 2010 lilitetewa na serikali ya israel kuwa ni halali kwa kuwa walikuwa wanalinda mipaka yao dhidi ya uingizwaji wa silaha haramu.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.