Israeli-Palestina

Waziri wa mambo ya nje wa Israel aonya kuhusu ombi la Palestina la kutaka uanachama wa UN

Waziri wa mamabo ya nje wa Israeli, Avigdor Lieberman.
Waziri wa mamabo ya nje wa Israeli, Avigdor Lieberman. Reuters

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Avigdor Lieberman amesema kuwa hakutakuwa na matokeo mazuri ikiwa Palestina itaendelea kung'ang'ania msimamo wake wa mpango wa kutafuta uanachama ndani ya Umoja wa Mataifa kama taifa huru.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza muda mfupi kabla ya mkutano wake na mkuu wa sera za nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, Lieberman hakuweka wazi juu ya madhara ya hatua hiyo, akisema kuwa muda haujawadia wa kutanabaisha ni kitu gani kitatokea.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi nchini humo, Ehud Barak mapema hii leo wamekutana na Ashton mjini Jerusalem.

Ofisi ya Netanyahu haijaweka wazi mazungumzo yao huku wizara ya ulinzi ikisema kuwa Ashton na Barak wamezungumza juu ya uhusiano wa Israel na Palestina.