Italia

Polisi ya Italia yakabiliana na wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa

Maandamano ya wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa
Maandamano ya wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa (CC) Antonello Mangano

Polisi wa kuzuia ghasia nchini Italia, wamekabiliana na mamia ya wakimbizi wa Tunisia katika kisiwa cha Lampedusa. Wakimbizi kadhaa waripotiwa kujeruhiwa katika purukushani hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Raia hao wa Tunisia wamekuwa wakiandamana, kupinga kile wanachokisema kuwa ni mazingira magumu katika kisiwa hicho.

Katika siku za hivi karibu ukosefu wa usalama umekuwa ukishuhudiwa katika kisiwa hicho katika mpaka wa Tunisia na Italia,huku zaidi ya wakimbizi elfu wakitaka kurejeshwa nchini Tunisia.

Zaidi ya wakimbizi,alfu arainaini wamekimbilia katika kiiswa hicho tangu mwanzo wa mawka ahuu hasa kutoka nchini libya na Tunisia.