Pata taarifa kuu
Ugiriki

Ugiriki na mbinu za kubana matumizi

Ujumbe kutoka: Ali Bilali
Dakika 1

Baraza la mawaziri nchini Ugiriki, linakutana baadaye hivi leo kujadili mbinu za kubana matumizi ya fedha, na kutangaza idara zikazoathirika, ili kujinasua katika hali ngumu ya kiuchumi inayokabiliana nayo kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wanaoshughulika na maswala ya mikopo kutoka katika Umoja wa Ulaya, wakindamana na wale kutoka shirika la fedha duniani IMF na benki kuu ya ulaya wanatarajiwa kuzuru Ugiriki na kufanya mazungumzo zaidi kuhusu swala hilo.

Kwa sasa Ugiriki, inahitaji Dola Bilioni 6 nukta 9 ili kulipa madeni ya kitaifa nchini humo,wakati pia ikitakiwa kupata zaidi ya Euro bilioni 2 kupitia kwa mfumo wa kubana matumizi, kushawishi umoja wa Ulaya na shiurika la fedha duniani IMF kuipamkopo wa Euro Bilioni 110.

Vyama vya wafanyakazi nchini humo vimetangaza maadanamano ya kitaifa dhidi ya mpangilio wa serikali kubana matumizi, mwezi ujao Tarehe 5 na 19.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.