Urusi

Waziri wa fedha wa Urusi aachishwa kazi

Waziri wa fedah wa urusi Alexei Kudrins
Waziri wa fedah wa urusi Alexei Kudrins REUTERS/Denis Sinyakov

Waziri wa fedha nchini Urusi Alexei Kudrins ambaye amekuwa katika nafasi hiyo toka mwaka 2000 amefukuzwa kazi na rais Dimitry Medvedev kufuatia matamshi yake ya kumkosoa waziri mkuu Vladimir Putin.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa rais Medvedev, amesema kuwa Kudrins hakujiuzulu kama ilivyoripotiwa badala yake aliachishwa kazi na rais kufuatia ushauri wa waziri mkuu Putin.

Uamuzi wa serikali hiyo kumfukuza kazi waziri huyo wa fedha inakuja kufuatia kiongozi huoy kuweka wazi kuwa hatakuwa tayari kufanya kazi chini ya uongozi wa rais Putin endapo atateuliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Tayari rais Medvedev ametangaza kutogombea nafasi ya urais hapo mwakani na hivyo kumpa nafasi waziri Mkuu Putin kutetea tena kiti hicho huku Medvedev akitarajiwa kurejea katika nafasi ya waziri mkuu.