Asia-Ulaya

Masoko ya Hisa Barani Asia yaimarika dhidi ya yale ya Ulaya

Masoko ya Hisa Barani Asia yameimarika katika siku ya pili ya mapambano yake dhidi ya yale ya Ulaya kitu ambacho kinatajwa kama onyo kwa Viongozi wa Bara hilo kuhakikisha inachukua hatua kukabiliana na mgogoro wa madeni uliopo. 

Matangazo ya kibiashara

Masoko ya Hisa ya Tokyo, Sydney, Shanghai na Seoul yamefanya vizuri katika biashara zake za asubuhi ya leo na swali limebakia ni kwa namna gani masoko ya Ulaya yatakavyokuwa baada ya kufunguliwa.

Hatua hii inakuja wakati hapo jana Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou ambaye alizuru nchini Ujerumani kuomba msaada wa kukwamuliwa kwenye matatizo waliyonayo akiahidi watafanya kila linalowezekana.