Umoja wa Ulaya

Tume ya jumuia ya Ulaya yatowa mapendekezo ya kifedha ya utozaji ushuru kwa mataifa wanachama

Mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso
Mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso REUTERS/Vincent Kessler

Tume ya jumuiya ya Ulaya, imetoa mapendekezo ya kifedha ya namna mataifa ya Ulaya yatatozwa ushuru, mpango ambao ikiwa utatekelezwa kuanzia mwaka wa 2014, basi huenda jumuiya hiyo ya EU ikakusanya zaidi ya Euro bilioni 50 kila mwaka. Rais wa tume hiyo Jose Manuel Barroso anasema, benki barani ulaya hazina budi kuchangia katika mpango,hasa wkaati huu ambacho jumuiya hiyo inavyokabliana na hali ngumu ya kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri,Barroso amewaambia wabuinge wqa jumuiya hiyo kuwa Ugiriki,itasalia katika jumuiya ya matifa ynayotumia sarafu ya Euro, lakini akaonya mkuwa hakika umoja huo kwa sasa unapitia wakati mgumu sana kifedha.

Waziri Mkuu wa Ugiriki,amekuwa nchini Ujerumani kuomba uungaji mkono wa nvchi hiyo kusaidia kurejesha hali ya kawaida,nchini humo wakati huu inapokabiliwa na deni kubwa,jambo amablo limesabisha maandamnao ya wannachi nchini humo wanaopiunga mpango wa serikali wa kubana matumizi.