Ugiriki

Uchumi wa Ugiriki kukaguliwa na wachunguzi wa kimataifa

AFP PHOTO/ Louisa Gouliamaki

Wakaguzi wa hesabu wa kimataifa wameelekea nchini Ugiriki, kwa ajili ya kutathimini hali ilivyo na namna Ugiriki inavyopambana na hali ya madeni nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya fedha yametangaza kuwa wakaguzi hao watamaliza kazi yao ndani ya wiki nne.

Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreau kutembelea nchini Ujerumani kuomba uungwaji mkono kwa kuwaambia wanasiasa na wafanyabiashara wa nchini humo kuwa nchi yake inafanya juhudi za kupambana na mzigo wa madeni walionao hivi sasa.

nayo Tume ya jumuiya ya Ulaya,imetoa mapendekezo ya kifedha ya namna mataifa ya ulaya yatatozwa ushuru, mpango ambao ikiwa utatekelezwa kuanzia mwaka wa 2014 basi huenda jumuiya hiyo ya EU ikakusanya zaidi ya Euro bilioni 50 kila mwaka.

Rais wa tume hiyo Jose Manuel Barroso anasema,benki barani ulaya hazina budi kuchangia katika mpango,hasa wakati huu ambacho jumuiya hiyo inakabiliana na hali ngumu ya kiuchumi.