Uingereza

Fergurson amuunga mkono Roberto Mancini kuhusu Tevez

Reuters/

Kocha wa klabu ya soka ya Uingereza Manchester United Alex Ferguson amemuunga mkono kocha wa Manchester City Roberto Mancini juu ya namna anavyoshughulikia suala la mchezaji arlos Tevez aliyegoma kucheza mechi wakati timu yake ikicheza na timu ya Bayern Munich katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Alex Ferguson amesema kuwa Manchini ametumia mamlaka yake na ameonyesha uwezo wa kiuongozi kitu ambacho ni muhimu sana katikamaendeleo ya soka katika ngazxi ya klabu na taifa kwa ujumla.

Wakati huohuo Makamu mwenyeki wa shirikisho la soka duniani,FIFA Bw.Jim Boyce amesema kuwa endapo itathibitishwa kuwa mchezaji Carlos Tevez alikataa kushiriki mechi dhidi ya Bayern Munich kama alivyotakiwa na kocha wake anaweza kukabiliwa na adhabu kali.

Mchezaji anaweza kukabiliwa na adhabu ya kuzuiliwa kucheza mchezo huo duniani kote hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha yake ya soka.

Kwa sasa mchezaji huyo amefungiwa kucheza soka kipindi hcha majuma mawili, huku klabu hiyo ikiendelea kumchunguza na mkataba wake unaweza kufutwa kama atakutwa na hatia.