UINGEREZA

Mahakama ya Uingereza yaamuru Assange kusafirishwa kwenda Sweeden kujibu tuhuma za ubakaji

Mmiliki wa kampuni ya Wikileaks Julian Assange akiwa amezungukwa na waandishi wa habari baada ya kutolewa kwa hukumu yake
Mmiliki wa kampuni ya Wikileaks Julian Assange akiwa amezungukwa na waandishi wa habari baada ya kutolewa kwa hukumu yake Reuters

Mahakama moja nchini Uingereza imetoa hukumu na kuamuru mmiliki wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange kusafirishwa kupelekwa nchini Sweeden kwenda kujibu mashtaka ya ubakaji yanayomkabili kiongozi huyo.

Matangazo ya kibiashara

Akisoma hukumu hiyo jaji John Thomas na Duncun Ousley wamesema kuwa Assange anawajibu wa kujibu tuhuma zinazomkabili nchini Sweeden na hivyo mahakama hiyo haioni sababu ya kuzuia mmiliki huyo wa mtandao unaoandika habari za uchunguzi kusafirishwa kwenda kujibu mashtka yanayomkabili.

Mahakama kuu nchini Sweeden ilitoa hati ya kukamatwa kwa mmiliki huyo wa Wikileaks na kupelekwa nchini humo kwaajili ya kujibu tuhuma za ubakaji zinazomkabili ambazo zilifunguliwa na wafanyakazi wake wawili wakike waliokuwa wakijitolea kufanya kazi kwenye kampuni yake.

Akiongea kabla ya hukumu hiyo wakili anayemtetea Assange, Julian Knowles amesema kuwa mteja wake anayo haki ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya nchi hiyo endapo hatoridhishwa na hukumu ya mahakama ambayo imesikiliza kesi hiyo.

Kwa upande wake bwana Assange amesema kuwa yeye anaamini hana hatia na makosa ambayo anatuhumiwa nayo na kwamba hajawahi kufanya vitendo vyovyote vya ubakaji katika nchi yoyoyte barani ulaya.

Aidha kiongozi huyo ameongeza hukumu iliyotolewa na majaji hao imechangiwa na nchi ya Marekani na Uingereza kushinikiza majaji hao kutoa huku ambayo wameitangaza.

Juma moja lililopita Assange mwenyewe alitangaza kampuni yake kusitisha kwa muda uchapishaji wa habari za uchunguzi kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha uliotokana na kuzuiliwa kwa mifumo ya fedha iliyokuwa inatumika kuchangia kampuni yake.