ITALIA

waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi kukabiliwa na shinikizo la kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi
Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi REUTERS/Alessandro Bianchi

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi anakabiliwa na zoezi la kupigwa kura juu ya Bajeti ya nchi hiyo huku kukiwa na hofu kuwa huenda Italia nayo ikakumbwa na mzigo wa madeni.

Matangazo ya kibiashara

Gharama za kukopa za serikali ya Italia zimeongezeka kwa kuhofu kushindwa kulipa madeni makubwa yaliyonayo.
 

Siku ya jumatatu Berlusconi aliyeshinda kura za kuwa na imani nae,alikana taarifa kuwa alipanga kujiuzulu. Huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa ikiwa Berlusconi atapoteza katika kura kuhusu bajeti yake,itakuwa vigumu kumuona tena akiwa tena madarakani kwa muda mrefu zaidi.
 

Katika hatua nyingine mawaziri wa fedha kutoka ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Brussels nchini Ubelgiji kwa ajili ya mazungumzo,huku suala la Italia hivi sasa likitawala zaidi kuliko la ugiriki ambapo viongozi wa kisiasa nchini humo wako katika mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja nchini humo na kuanzisha mchakato mpya wa kubana matumizi ili kupata mkopo kutoka kwa mashirika ya fedha ya kimataifa.