Ugiriki

Wagiriki wasubiri kutangazwa jina la waziri mkuu

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias akiwapokea Georges Papandréou pamoja na mkuu wa upinzani Antonis Samaras ikulu ya rais jijini  Athènes, Novemba 6, 2011.
Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias akiwapokea Georges Papandréou pamoja na mkuu wa upinzani Antonis Samaras ikulu ya rais jijini Athènes, Novemba 6, 2011. REUTERS/John Kolesidis

Jina la waziri mkuu mpya nchini Uturuki huenda likatangazwa baadae leo mchana, baada ya viongozi wa vyama vikuu kuafikiana kuunda serikali ya muungano itayo kuwa na jukumu la kuhakikisha mgogoro wa kiuchumi unaolikumba taifa hilo unapatiwa jawabu maridhwawa.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa viongozi hao uliahirishwa jana na kupangwa kufanyika alhamisi hii

Antonis Samaras, mkuu wa chama cha upinzani amelaumu chama cha wa socialist kuchelewesha harakati za kumtangaza waziri mkuu mpya baada ya kujiuzulu kwa Georges Papandreu.

Wakati akitowa hutuba yake ya mwisho hapo jana, waziri mkuu anaeondoka madarakani George Papandreu amesema kwamba wameafikiana kuhusu jina la waziri mkuu ambae atakuwa tayari kuwaweka pamoja wafuasi wa vyama tofauti, na kuhakikisha wanasalia kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya.

George Papandreu amesema atajiuzulu pale tu jina la waziri mkuu mpya litapo tangazwa