UGIRIKI

Waziri mkuu mpya wa Ugiriki atangazwa

Waziri mkuu mpya wa Ugiriki Lukas Papademos
Waziri mkuu mpya wa Ugiriki Lukas Papademos REUTERS/Yiorgos Karahalis

Hatimaye mara baada ya mjadala wa muda mrefu kati ya viongozi wa upinzani na wale wa chama Tawala nchini Ugiriki hii leo wamemaliza tofauti zao na kumpitisha kwa kauli moja aliyekuwa makamu wa rais wa benki ya umoja wa Ulaya Lucas Papademos kuwa waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya George Papandreou aliyejiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Kutangazwa kwa jina hilo kunamaliza sintofahamu iliyokuwa imetawala hapo awali kuhusu kupatikana kwa mrithi wa kiti hicho ambapo sasa rais wa Ugiriki Caralos Papoulias amemdhibitisha rasmi Papademos kuwa waziri mkuu na kumuagiza kuunda serikali mpya.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa papademos huenda akawa kiongozi bora kutokana na uzoefu wake wakati akiwa makamu wa rais wa benki ya umoja wa Ulya na jinsi alivyoweza kusimamia suala la uchumi wa nchi wanachama wa Umoja huo.