ITALIA

Bunge la Italia kupiga kura hii leo kupitisha mpango mpya wa kubana matumizi.

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi
Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi

Bunge la nchini Italia linapiga kura hii leo juu ya mpango wa kubana matumizi,sharti lililotolewa na umoja wa ulaya ili kuiepusha Italia na mzigo wa madeni. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kubana matumizi huenda ikaungwa mkono na kufungua milango kwa waziri mkuu wa nchi hiyo,Silvio Berlusconi kujiuzulu.

Berlusconi,aliyepoteza kura nyingi siku ya jumanne,kura zilizoonesha kutokuwa na imani nae,aliahidi kujiuzulu mara baada ya kupitishwa kwa mpango wa kubana matumizi na Mabunge nchini humo.

Katika hatua nyingine, Rais wa Marekani, Barack Obama amezungumza na rais wa Italia, Giorgio Napolitano na kusema kuwa ana imani na utawala wake wakati huu nchi hiyo inapopambana na changamoto ya kisiasa na uchumi.

Afisa wa zamani kutoka umoja wa ulaya na Mchumi maarufu Mario Monti ameibuka na kupewa nafasi kuwa pengine anaweza kuchukua nafasi ya waziri mkuu Berlusconi huku kukiwa na matumaini ya kupata ufumbuzi wa mzigo wa madeni kupitia kwa serikali mpya itakayoundwa.