Italia

Nahodha wa Meli iliyopinduka nchini Italia, atolewa Mahabusu

Meli Kubwa iliyopinduka pwani ya magharibi ya  Italia
Meli Kubwa iliyopinduka pwani ya magharibi ya Italia 路透社

Nahodha wa Meli ya Costa Concordia ya nchini Italia ameachiwa huru kutoka mahabusu na kuwekwa kizuizini akiwa nyumbani kwake mjini Meta di Sorrento.

Matangazo ya kibiashara

Francesco Schettino,anayeshutumiwa mauaji ya bila kukusudia na kutelekeza meli kabla ya Abiria kuokolewa amerejeshwa nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi wa Maafisa wa Polisi.

Mamlaka ya Bandari ilinasa sauti ya Mazungumzo ya njia ya simu yaliyoonesha Schettino akipuuza amri ya kurudi chomboni baada ya chombo hicho kugonga Mwamba.
 

Idadi ya watu waliopteza maisha kwenye ajali ya Meli imefikia watu kumi na mmoja baada ya Kikosi cha Uokoaji kufanikiwa kupata miilimingine mitano.