Ufaransa-Uchaguzi

Rais Sarkozy amshambulia mpizani wake Francois Hollande wakati wa kampeni ya uchaguzi

Nicolas Sarkozy akilakiwa na wafuasi wa chama chake jijini Marseille, jumapili 19 Februari 2012.
Nicolas Sarkozy akilakiwa na wafuasi wa chama chake jijini Marseille, jumapili 19 Februari 2012. REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameendesha kampeni ya uchaguzi jana jumapili katika mji wa Marseille ikiwa ni siku ya pili ya kampeni zake za kutetea wadhifa wake na kuwataka wananchi wa taifa hilo kuendelea kumuunga mkono kwenye harakati zake ili aweze kumalizia kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika hutuba yake Rais Sarkozy amewasihi wafuasi wake kuhakikisha wanasimama pamoja kuwaunganisha wananchi wa Ufaransa pamoja na kushughuliaki suala la uchumi linaloonekana kusuasua.

Akiwahutubia halaiki ya wafuasiwa chama chake, Nicolas Sarkozy amekishambulia chama cha upinzani cha ki Socialist na kumlinganisha kiongozi wa chama hicho Francois Hollande kama mtu ambae anataka kuididimiza Ufaransa, huku akimuita muhaini.

Watu zaidi ya elfu kumi wanatajwa kujitokeza kwenye kampeni hizo huku wakiwa na bendera za Chama hicho cha Kisoshaliti wakiimba nyimbo za kumnadi Sarkozy kama mshindi dhidi ya mpinzani wake Francois Hollande.