Ufaransa

Kiongozi wa zamani wa IMF Dominique Strauss Kahn azuiliwa na polisi

Kiongozi wa zamani wa IMF Dominique Strauss Kahn akiziuliwa na polisi nchini Ufaransa
Kiongozi wa zamani wa IMF Dominique Strauss Kahn akiziuliwa na polisi nchini Ufaransa REUTERS/Benoit Tessier

Polisi wa Ufaransa wanamshikilia aliyekuwa mkuu wa taasisi ya kimataifa ya fedha IMF Dominique Strauss-Kahn kwa tuhuma za kuhusika katika biashara za ngono zilizoandaliwa na wafanyabiashara huko Paris na Marekani. 

Matangazo ya kibiashara

Strauss-Kahn ambaye hadi mwaka jana amekuwa akionekana kuwa mstari wa mbele kama mrithi wa rais Nicolas Sarkozy katika kiti cha urais nchini Ufaransa amekuwa akitaraji kuhojiwa kama shahidi lakini kwa sasa wanaendesha mashataka wamesema kuwa atahojiwa kama mtuhumiwa.

Khan amewasili katika kituo cha polisi katika mji wa Kaskazini wa Lille kabla ya miadi yake asubuhi ya leo kwa mahojiano kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya ngono ya hivi karibuni ambayo inatia dosari zaidi katika taaluma yake.

Muda mfupi baada ya kuwasili waendesha mashtaka wamesema kuwa Khan atashikiliwa kwa saa 96 kwa uchunguzi kuhusu tuhuma za kuhusika katika biashara ya ngono na ubadhirifu wa fedha za kampuni na kwamba huenda akawa na kesi ya kujibu.

Baada ya uchunguzi huo kama majaji wataridhia huenda akasalia katika mahabusu kungoja kesi yake au ataachiwa kwa dhamana.