UGIRIKI

Wakopeshaji binafsi bado wachelea kuisadia nchi ya Ugiriki wakati muda wa kufanya hivyo ukifika tamati leo

Nchi ya ugiriki inatakiwa kuwa imepatiwa mkopo kabla ya tarehe 20March 2012
Nchi ya ugiriki inatakiwa kuwa imepatiwa mkopo kabla ya tarehe 20March 2012 Reuters/Yiorgos Karahalis

Ikiwa leo ni siku ya mwisho ambayo wakopeshaji binafsi nchini Ugiriki wanapaswa kuwa wameshaipatia fedha za mkopo nchi hiyo bado hali inaonekana kuwa ngumu kwa serikali ya waziri mkuu Papademos. 

Matangazo ya kibiashara

Utata huo unaibuka kufuatia hofu ambao imetangazwa na wakopeshaji hao ambao wamedai hawana imani na mfumo mpya ambao umetangazwa na Serikali kwaajili ya matumizi ya fedha hizo.

Wakopeshaji hao ambao wanatarajiwa kutoa kiasi cha Euro bilioni 100 ili kukamilisha mkopo wa zaidi ya Euro bilioni 350 ambao nchi hiyo inatakiwa kupatiwa kwa lengo la kujikwamua na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo.

Hapo jana taasisi ya fedha inayosimamia benki kwenye Umoja wa Ulaya EU ya IIF ilitoa ripoti maalumu ambayo inaonyesha jinsi Serikali ya Ugiriki inavyoendelea kushughulikia mdororo wa kiuchumi na mikakati iliyojiwekea kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Endapo wakopeshaji hao binafsi watachelewesha utoaji wa fedha hizo huenda ukaathiri mfumo mzima wa fedha kwenye Serikali ya waziri mkuu Lucas Papademos ambayo inategemea fedha hizo kwaajili ya kukabilina na deni kubwa ambalo linaikabili nchi hiyo.