OSLO-NORWAY

Breivik: Nilitarajia kutekeleza mauaji zaidi ya niliyoyatekeleza

Mtuhumiwa wa mauaji nchini Norway, Anders Breivik
Mtuhumiwa wa mauaji nchini Norway, Anders Breivik Reuters

Kijana ambaye amekiri kufanya mashambulizi nchini Norway na kuua watu sabini na saba Anders Behring Breivik ameiambia Mahakama ambayo inasikiliza shauri lake alikuwa na lengo la kuuwa wanafunzi wote na kilichomshawishi ni kucheza michezo kama ilivyo kwenye video. 

Matangazo ya kibiashara

Breivik bila ya kung'ata maneno akiwa katika Mahakama ya Oslo katika siku yake ya nne ya kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya mauaji ambayo inamkabili amesema nia yake ilikuwa ni kuua mamia ya aliowalenga kwenye Kisiwa Cha Utoeya.

Kijana huyo ambaye ana msimamo mkali amesema mwaka elfu mbili na sita alikuwa akifanya mazoezi ya taamuli nchini Japan pamoja na kucheza video game ambazo zinaonesha namna ya kufanya mashambulizi ambapo mtu mmoja anaweza kumuua mamia ya watu.

Kesi hiyo imeendelea kuzusha masuala mapya kuhusu kesi hiyo na dhamira aliyokuwanayo mtuhumiwa huyo kutekeleza mauaji ambayo aliyafanya.

Upande wa mashtaka umeendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ambaye hii leo kesi yake inaingia siku ya tano na ataendelea kuoa ushahidi zaidi kuhusu ni kwanini aliamua kutekeleza mauaji aliyoyafanya.

Wataalamu wa masuala ya akili wameendelea kuwa na wasiwasi kuhusu akili ya Breivik ambaye awali walisema hakuwa na akili timamu kabla ya majuma kadhaa yaliyopita wataalamu wengine kudai kuwa mtuhumiwa huyo ana akili timamu.