Shinikizo zaidi kutoka IMF kwa mataifa ya Ulaya kuhusu kukabiliana na mdororo wa Uchumi

Mkuu wa fuko la fedha duniani IMF Christine Lagarde
Mkuu wa fuko la fedha duniani IMF Christine Lagarde Reuters/路透社

Shirikisho la fedha duniani IMF limeendelea kuongeza shinikizo zaidi kwa mataifa ya Ulaya kuhakikisha kuwa nchi hizo zinachukua hatua mathubuti kukabiliana na mdororo wa kiuchumi ambao umeendelea kutikisa kanda ya Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yamebainishwa na shirika hilo wakati viongozi wake walipokutana na wawakilishi wa mataifa tajiri duniani ambao ni wachangiaji wakubwa wa shirika hilo kifedha ambapo wameyataka mataifa hayo kuhakikisha wanapata zaidi ya dola bilioni 430.

mkurugenzi wa shirika hilo Christine Lagrade amesema kuwa licha ya kuwa uchumi umeanza kuimarika kwenye baadhi ya nchi lakini uwajibikaji wa viongozi wake ni suala la muhimu katika kluhakikisha wanakusanya kiasi hicho cha fedha.

shinikizo toka IMF limekuja baada ya mataifa yaliyosimama kiuchumi kwasasa duniani nchi za China, Brazil, India na Urusi kukubali kutoa kiasi cha fedha kwenye shirika hilo kwa lengo la kusaidia mataifa yaliyotumbukia kwenye mtikisiko wa uchumi.