Ugiriki

Chama cha mrengo wa Kushoto nchini Ugiriki,Syriza chatangaza kutoshiriki Mazungumzo ya hii leo

Rais wa Ugiriki, Carolos Papoulias
Rais wa Ugiriki, Carolos Papoulias

Kiongozi wa Chama cha Syriza cha mrengo kushoto nchini Ugiriki Alexis Tsipras ametangaza kutoshiriki kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano nchini humo kitu ambacho kinaongeza mgogoro mkubwa wa utawala katika nchi hiyo kwa majuma mawili sasa.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa nchi hiyo, Carolos Papoulias hii leo alitarajia kuwa na mazungumzo baada ya kura za May 6 ambapo wapigakura walivikataa vyama vikubwa nchini humo vilivyokuwa vikiunga mkono mpango wa kubana matumizi uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha Duniani, IMF.
 

Mazungumzo hayo ambayo yatafanyika nyumbani kwa rais Karolos Papoulias sasa yatavikutanisha Chama cha mrengo wa kulia cha New Democracy na kile cha Kisoshalisti cha Pasok ambavyo vitaendelea na juhudi za kuunda serikali.
 

Vyama hivyo viwili vinawiana kwenye mchakato wa kuutekeleza mapendekezo ya Umoja wa wa Ulaya EU na Shirika la Fedha Duniani IMF ambalo linataka wabane matumizi na hapa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Masinde Murilo Brian Wanyama anatupia jicho mgogoro huu.
 

Ikiwa uundwaji wa Serikali mpya utashindwa kufua dafu siku ya Alhamisi, uchaguzi mpya hautakuwa na budi kuitishwa kwa ajili ya zoezi la kupiga kura mwezi June.