Hollande aapishwa hii leo kuwa Rais wa Ufaransa
Kiongozi wa chama cha kisoshalisti nchini Ufaransa Francois Hollande, ameapishwa kuwa Rais wa 24 wa Ufaransa baada ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy kuachia madaraka baada ya kushindwa kwenye duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi nchini humo. Shamrashamra za kuapishwa kwake zilizofanyika katika Kasri la Champs Elysees jijini Paris.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kama ilivyo ada rais anaeacha madaraka alimsubiri rais mteule na baadae kumuelekeza hadi Ikulu na kisha kukutana nae kwa dakika kadhaa na baadae rais mteule akamshindikiza rais alieondoka madaraka hadi nje na baadae kurejea ukumbini kuendelea na shughuli.
Akizungumza baada ya kuapishwa kwake, Hollande amesema kuwa anataka kufungua mlango mpya barani Ulaya na kuongeza kuwa hayo ndio kazi aliyopewa na Raia wa nchi hiyo katika Kura za May 6.
Hollande ameahidi kuiweka Ufaransa katika Misingi ya Utawala wa Sheria, na kuchangia katika kuimarisha amani ya Dunia na kuilinda.