Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande aahidi kushirikiana na Ujerumani kupambana na tatizo la kiuchumi

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel REUTERS/Jacky Naegelen

Rais Mpya wa Ufaransa Francois Hollande amejipiza kuhakikisha anashirikiana na Ujerumani katika kusaka suluhu ya mgogoro wa kiuchumi ambao unashuhudiwa kuyakumba mataifa ya Ulaya kitu kilichochangia kuchukuwa kwa hatua za kubana matumizi.

Matangazo ya kibiashara

Rais Hollande ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake ya kwanza huko Berlin muda mchache baada ya kuapishwa na kukutana na Kansela Angele Merkrl ambapo kwa pamoja wakasema ushirikiano wa mataifa hayo utaendelea kunusuru uchumi wa Ulaya.
 

Mapema kabla hajaelekea Berlin Rais Hollande alimtangaza Jean-Marc Ayrault kuwa Waziri Mkuu wake na kisha kuanishi majukumu ambayo atakabiliana nayo kwenye serikali yake ikiwemo ajira na ukuaji mdogo wa uchumi.