Ugiriki

Ugiriki yajiandaa kufanya Uchaguzi Mwezi Juni Mwaka huu

REUTERS/Aris Messinis/Pool

Ugiriki inajiandaa kurejea kwenye uchaguzi mwingine katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya mazungumzo ya kutaka kuunda serikali ya Muungano kugonga mwamba kwa mara nyingine.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe kumi na saba mwezi Juni hatua inayokuja baada ya vyama vyenye wingi wa wabunge nchini Ugiriki kushindwa kufikia muafaka wa kuunda serikali kutokana na kutofauti kwenye sera ya kubana matumizi.
 

Kiongozi wa Chama Cha Kisoshalisti cha Pasok, Evangelos Venizelos amesema wanakwenda kwenye uchaguzi mwingine wakati hali ikiendelea kuwa mbaya kutokana na kushindwa kufikiwa muafaka na watu kupuuza umuhimu wa nchi.
 

Rais Carolos Papoulias anatarajiwa kukutana kwa mara nyingine na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kwa ajili ya kuchagua utawala wa muda kabla ya nchi hiyo kujianda kwa uchaguzi mwingine wa wabunge.
 

Ujerumani na Ufaransa zimejiapiza kuhakikisha vinavalia njuga suala la kumaliza kwa mgogoro wa kiuchumi unaoendelea Barani Ulaya kauli ambayo imetolewa na Rais Francois Hollande na Kansela Angela Merkel.