Uholanzi

Kesi ya Kiongozi wa zamani wa Jeshi la Serbia Ratko Mladic yaahirishwa baada ya makosa katika uwasilishaji wa ushahidi

Kiongozi wa zamani wa majeshi ya Serbia, Ratco Mladic
Kiongozi wa zamani wa majeshi ya Serbia, Ratco Mladic AFP / TPIY

Mahakama maalumu inayosikiliza kesi dhidi ya Jenerali wa zamani wa Serbia Ratko Mladic imesimamisha kwa muda kusikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mashataka kukiri kufanya makosa katika kuwasilisha ushahidi dhidi ya Mladic. 

Matangazo ya kibiashara

Jaji kiongozi wa kesi hiyo Alphons Orie ametangaza uamuzi huo hapo jana wakati akihiarisha shauri hilo na kusema kuwa kuna vipengele ambavyo ni dhahiri kuwa upande wa mashtaka ulikiuka kwa kutoa baadhi ya ntyaraka za ushahidi kwa upande wa utetezi.

Upande wa utetezi umeomba kesi hiyo iahirishwe kwa miezi sita ambapo jaji Orie amesema atafikiria ombi la upande wa utetezi lakini majaji wamepanga kuanza kusikiliza tena kesi hiyo mapema iwezekanavyo.

Wakati kesi hiyo ikiahirishwa upande wa mashtaka ulikuwa ukiwasilisha ushahidi wake wa awali kuhusu mauaji vijana waislamu zaidi ya elfu 7.