Uingereza

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon awataka wanachama wa ukanda wa Euro kuchukua hatua kupambana na tatizo la uchumi

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron hii leo amerejea tena wito wake kwa viongozi wa nchi wanaotumia Sarafu ya Euro kuchukua hatua madhubuti za kupambana na tatizo la kiuchumi, au la kuingia katika hatari ya kuanguka kwa Sarafu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba aliyoitoa Mjini Manchester, Cameron ametaka nchi Wanachama 17 wa ukanda wa Euro ambao Uingereza si Mwanachama kuunga mkono Mpango wa kubana Matumizi.

Cameron amekiri kuwa Ujumbe wake huo utawapa Ghadhabu viongozi wengi lakini amesema kipaumbele kwake ni kuilinda Uingereza, kwa kuwa ukanda huo uko kwenye hali ya hatari kiuchumi.

Hofu ya Ugiriki kuondolewa kutoka Ukanda huo zimezidi kuongezeka baada ya Kura zilizopigwa May 6 kuunga mkono vyama vinavyopinga Sera ya kubana Matumizi .

Benki kuu nchini Uingereza ilionya kuwa hali ya mzigo wa Madeni ni tishio kubwa kwa Uchumi wa Uingereza, hata kama tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi.