ROMANIA

Waziri wa mambo ya ndani wa Romania ajiuzulu wadhifa wake

Romania's President Traian Basescu takes notes before the Parliament vote on suspending him over what the ruling Social Liberal Union (USL) says is his attempt to pressure judges and break the constitution, in Bucharest July 6, 2012.
Romania's President Traian Basescu takes notes before the Parliament vote on suspending him over what the ruling Social Liberal Union (USL) says is his attempt to pressure judges and break the constitution, in Bucharest July 6, 2012. Reuters/路透社

Waziri wa mambo ya ndani wa Romania, Ioan Rus ametangaza kujiuzulu nafasi yake kufuatia tuhuma kuwa alihusika kwa kiasi kikubwa kuweka shinikizo la kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Traian Basescu.

Matangazo ya kibiashara

Rus amesema kuwa tayari amewasilisha barua ya kujiuzulu wadhifa wake kwa waziri mkuu Victor Ponta ambaye nae amekiri kupokea barua hiyo na kuikubali.

Rus pamoja na naibu wake Victor Dobre ndio ambao wametajwa kuweka shinikizo kubwa la kuitishwa kwa kura ya kutokuwa na imani na rais majuma kadhaa yaliyopita kura ambayo hata hivyo rais Basescu alishinda na kuendelea kubakia madarakani.

Toka kuitishwa kwa kura hiyo kumekuwa na hali ya sintofahamu kwenye siasa za nchi hiyo na kutishia kuvunjika kwa serikali ya muungano ambayo inaundwa na vyama vya upinzani.

Juma lililopita mahakama kuu ya nchi hiyo iliahirisha kutoa hukumu kuhusu kesi iliyofunguliwa mahakamani dhidi ya viongozi ambao waliitisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais ambapo walikuwa wanahoji uhalili wa kupigwa kwa kura hiyo.