Australia

Waziri wa Australia azungumzia sakata la Julian Assange

REUTERS/Olivia Harris

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Australia, Bob Carr amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kesi inayomkabili mmiliki wa mtandao wa wikileaks Julian Assange.

Matangazo ya kibiashara

Waziri amedai kuwa kulikuwa na uwezekano mdogo kwa nchi ya Sweeden kumhamishia mtuhumiwa huyo Marekani.

Assange ameomba hifadhi ya kisiasa kwa nchi ya Ecuador iliyokubali kumpatia hifadhi hiyo akidai kuwa kuna mpango wa yeye kupelekwa nchini Sweeden kujibu tuhuma za ubakaji zinazomkabili lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa kuhamishiwa nchini Marekani.

Rais wa Ecuador Rafael Correa amesema kuwa kama isingekuwa kitisho cha kupelekwa marekani ambako anaweza kuhukumiwa kifo au kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi basi bwana Assange angekubali kirahisi kupelekwa nchini Sweeden.

Serikali ya Australia imekuwa ikikosolewa kutokana na kukaa kimya kuhusu kesi inayomkabili Assange ambaye ni raia wake.