Serbia

Kiongozi wa zamani wa majeshi ya Serbia ajitetea mahakamani

Kiongozi wa zamani wa majeshi ya Serbia Radovan Karadzich akijitetea mahakamani
Kiongozi wa zamani wa majeshi ya Serbia Radovan Karadzich akijitetea mahakamani ICTY via Reuters TV

Kamanda wa zamani wa majeshi ya Serbia Radovan Karadzich ambaye anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita leo Jumanne ametoa utetezi wake dhidi ya tuhuma zinazomkabili katika mahakama ya uhalifu wa kivita huko The Hague Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Radovan Karadzich ameiambia mahakama hiyo kuwa anastahili kupongezwa kwa kuzuia vita nchini Bosnia na kupunguza ukiukwaji wa haki za binadamu huku akisisitiza kuwa hakuna mtu aliyedhani kuwa kungetokea mauaji ya kimbari dhidi ya raia wasio wa Serbia.

Akionekana mtulivu ndani ya vazi la suti wakati akitoa utetezi wake huku akitabasamu kwa vipindi, maneno yake yalikutana na vilio na vicheko vya chini chini vya raia na jamaa za watu waliosalimika, kuashiria kutosadiki kile anachozungumza.

Karadzich anatuhumiwa kuwa mmoja wa vinara wa kuratibu mipango iliyosababisha mauaji ya watu wapatao laki moja, na kuwaondoa wengine milioni moja katika makazi yao,katika vita vya Bosnia mwaka 1990.

Karadzic anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha jela iwapo atapatikana na hatia.