Pata taarifa kuu
SWEDEN-IRAN

Sweden yamtaka balozi wa Israel nchini humo kujieleza kuhusu matamshi ya kiongozi wa Israel dhidi ya serikali Sweden.

REUTERS/Francois Lenoir
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
1 Dakika

Serikali ya Swiden imemuita balozi wa Israel jijini Stockholm baada ya matamshi ya kiongozi mmoja wa israel ambae hakutambulika aliesema kwamba serikali ya Swiden itapinga muswada wa kuongeza vikwazo dhidi ya serikali ya Iran, ili , kulinda kampuni ya Swiden.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Swiden amefahamisha kwamba balozi wa Israel ametakiwa kijieleza kuhusu matamshi ya kiongozi huyo ambayo hata hivyo yanakisiwa kuwa ni kutoka wizara ya mambo nje ya Israel.

Gazeti moja la Israli la Haarets ambalo lilitaja chanzo cha serikali ya Israel na kuthibitisha kuwa Swiden inaendesha mbinu za kukwamisha juhudi za kuongeza vikwazo vya Umoja wa Ulaya ili kuruhusu uwepo wa mkataba baina ya kampuni ya telecoms Ericsson na kampuni ya Irancell.

Waziri wa Swiden wa mambo ya nje Carl Bildt akiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya jijini Luxembourg, amesema kwamba hakika habari hizi ni za uchochezi hazina ukweli wowote, na kusema kuwa serikali yake itatowa tamko dhidi ya Israel.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.