Uingereza

Watu wawili wafariki baada ya Helkopta kuanguka na kushika moto London Uingereza

RFI

Watu wawili wamefariki duniani baada ya Helikopta waliokuwa wanasafiria kugonga mnara na kuanguka kabla ya kushika moto jijini London Uingereza.Walioshuhudia ajali hiyo wanasema moto kutoka kwenye helikopta hiyo pia uliteketeza magari yaliyokuwa katika eneo hilo la River Thames huku mtu mwingine mmoja aliyekuwa amejeruhiwa akikimbizwa hospitalini.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi awali wa polisi uonaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni ukungu uliokuwa umetanda hewani na kusababisha mnara huo kutoonekana vema na rubani wa ndege hiyo.

Aidha, polisi wamefutulia mbali uvumi kuwa huenda mkasa huo ulikuwa umepangwa na magaidi.

Kwingine nchini Japan ndege za abiria aina ya Boeing 787 zimelazimika kutua kwa dharura na kusitisha safari zake kutokana na tatizo la kiufundi.

Mamlaka ya safari za ndege nchini humo imetanaga kuwa kuanzia leo itasitisha safari za ndege zingine saba za abiria kwa hofu ya kuzuka kwa tatizo kama hilo.

Hii si mara ya kwanza kwa ndege za abiria nchini humo kukumbwa na hitilafu ya kimitambo huku ikikumbukwa kuwa tatizo la kuvuja kwa mafuta na matatizo ya umeme pia lilikumba ndege hizo.