Pata taarifa kuu
DAVOS-USWIS

Mkuu wa IMF ataka dunia ijizatiti kukabiliana na matatizo ya uchumi

AFP PHOTO / STRINGER
Ujumbe kutoka: Flora Martin Mwano
Dakika 1

Mkuu wa Shirika la Fedha duniani IMF Christine Lagarde ametoa wito kwa mataifa mbalimbali duniani kutobweteka na badala yake waendeleze mikakati ya kukuza uchumi ili kukabiliana na matatizo yanayoikumba dunia kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Lagarde ametoa wito huo wakati akifunga mkutano wa kimataifa wa uchumi uliomalizika jumamosi hii mjini Davos Uswisi na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa dunia wakiwamo Marais toka nchi arobaini na tano, Wafanyabiashara, Wasomi na Waandishi wa Habari.

Awali katika mkutano wa mwaka huu mwanzilishi wa jukwaa la WEF Klaus Schwab aliwataka washiriki kujikita katika mikakati mipya ya kuimarisha uchumi wa Ulaya ambao unaendelea kuwa tete sambamba na ule wa nchi zinazoendelea hususani katika bara la Afrika.

Mkutano huo umemalizika huku Umoja wa Ulaya EU ukiwa katika msuguano baada ya Uingereza kueleza nia yake ya kutaka kujitoa katika umoja huo huku baadhi ya nchi wanachama wakiendelea ku

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.