Vatican

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani kuachia uongozi wake hii leo

Baba mtakatifu Benedikti wa 16
Baba mtakatifu Benedikti wa 16 REUTERS/Alessandro Bianchi

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto wa kumi na sita anajiuzulu leo Alhamisi baada ya kuahidi kufanya hivyo mapema mwezi huu kwa sababu ya umri wake mkubwa na sababu za kiafya zinazomnfya kutoendelea katika wadhifa huo.

Matangazo ya kibiashara

Jana Jumatano kiongozi huyo aliongoza misa yake ya mwisho katika Makao Mkauu ya Kanisa hilo mjini Vatican na kuwaaga maelfu ya watu waliokuja kumsikiliza.
Baada ya kujiuzulu kwake mchakato wa kumpata Papa mpya unaanza.
 

Kujiuzulu kwa Baba mtakatifu Benedikti hii leo kunafungua milango kwa nafasi hiyo ya juu kuwakutanisha makadinali takriban 115 kutoka ulimwenguni kote kwa ajili ya kuchagua mrithi.

Waangalizi wanaoutupia macho uteuzi huu wana matumaini kuwa Papa atakayepatikana anatarajiwa kutupia macho kwa ukaribu maswala ambayo yamekuwa Changamoto katika Kanisa hilo, hasa Mapenzi ya jinsia moja, matumizi ya Kondomu na Ndoa kwa Viongozi wa Dini.