ITALIA

Viongozi wa Mataifa yenye nguvu duniani yanakutana kuweza kuijadili Syria

Rais wa Ufaransa, Froncois Hollande akiwa katika Ziara yake mjini Moscow amesema anaamini juu ya kupata suluhu la kisiasa juu ya mgogoro wa Syria majuma kadhaa yajayo.

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo amesema hayo yatafikiwa kutegemea na msimamo wa Rais Vladmir Putini wa Urusi na Msimao wao pia na kueleza kuwa ni budi mazungumzo ambayo bado hayajaanza yaanze nchini Syria.
 

Hollande amesema kuwa alidhamiria kujadili mabadiliko ya kisiasa nchini Syria na ameona kuna uhitaji kwa Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuachia ngazi .
 

Hollande amesisitiza kuwa Ufaransa kama ilivyo kwa mataifa ya magharibi, imekuwa ikimtaka Assad kuachia uongozi huku Msimamo wa Urusi ukisema kuwa Raia wa Syria ni budi wakachagua weneywe Mustakabali wa nchi hiyo.
 

Katika hatua nyingine Mataifa yenye nguvu duniani wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Upinzani wa Syria mjini Roma hii leo baada ya Washington kusema kuwa iko tayari kutoa msaada kwa Waasi kupambana na utawala wa Assad.
 

Mazungumzo ya mjini Roma yamekuja siku mbili kabla ya mkutano ambao ni wa muhimu sana kwa upinzani mkutano unaotarajiwa kufanyika mjini Instambul nchini Uturuki ambapo upinzani huo unatarajiwa kuteua Waziri Mkuu na Serikali ili kuongoza Maeneo ya Syria ambayo yanashikiliwa na Upinzani.