Urusi

Putin aagiza mahakama kuendeleza vita dhidi ya makundi yenye itikadi kali

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Reuters / RIA Novosti

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewaamuru waendesha mashitaka nchini humo kuwa makini na makundi yenye msimamo mkali, ambayo amesema yamekuwa yakiendesha shughuli zao kwa wingi na bila aibu. 

Matangazo ya kibiashara

Putin ametoa kauli hiyo mbele ya jopo la waendesha mashitaka mjini Moscow akirejelea takwimu za matukio ya uhalifu kwa mwaka 2011 ambapo kwa asilimia 12% yalifanywa na makundi hayo na hivyo amesisitiza vita dhidi yao.

Hata hivyo Putin hakusema wazi hasa ni kundi gani analolizungumzia ingawa mahakama pia imetoa video ya vurugu zilizotokea huko Pussy ikiwaonesha wafuasi wawili waliofungwa kwa kufanya maandamano kanisani dhidi ya Putin.

Katika machafuko ya harakati za maandamano ya upinzani dhidi ya serikali bunge la Urusi lilipitisha sheria ambayo inaruhusu serikali kufungia tovuti ambazo zimeshindwa kuondoa itikadi za kimlengo bila kupitia hatua za mahakama.