UINGEREZA

Uingereza yataka Argentina waheshimu uamuzi wa wakazi wa kisiwa cha Falkland

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameitaka Argentina kuheshimu matakwa ya wakazi wa kisiwa cha Falkland baada ya raia hao kuamua kuwa sehemu ya Uingereza. Katika kura za maoni zilizopigwa kuhusu hadhi ya kisiasa ya kisiwa hicho na matokeo yake kutangazwa ziliafikia kuwa raia wake wameamua kuwa hadhi ya kisiasa hicho itabaki kuwa ya Uingereza.

Reuters/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Cameron amesema asilimia kubwa ya raia wa kisiwa hicho wamekubali kuwa sehemu ya Uingereza hivyo Argentina na watu wote wanapaswa hawapaswi kuingilia uhuru wa wahusika wenyewe.

Asilimia 99.8 ya wakazi hao walipiga kura ya kubakia kuwa sehemu ya Uingereza kati ya asilimia 92 ya watu wote waliojitokeza katika zoezi hilo.

Kisiwa cha Falkland kimekuwa kikigombaniwa na Uingereza na Argentina na maamuzi hayo yamefikiwa baada ya zoezi la kura ya maoni kufanyika katika mamlaka kisiwani humo chini ya waangalizi wa ndani, waangalizi wa kimataifa na vyombo vya habari.

Mvutano wa kisiwa hicho ulisababisha vita kwa takribani majuma kumi kati ya Argentina na Uingereza mnamo mwaka 1982 na baadaye kisiwa hicho kuwa chini ya Uingereza.