IRAN

Rais wa Iran aanza ziara barani Afrika

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad RFI

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad leo Jumapili ameanza ziara katika mataifa ya Afrika ikiwemo Benin, Ghana na Niger huku mikataba ya nishati ikiwa ni ajenda muhimu.  

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuondoka mjini Tehran Ahmadinejadi amekaririwa akisema kuwa katika ziara hiyo mbali na kuimarisha mahusiano baina yake na mataifa hayo lakini pia watakuchukua hatua ndefu katika kukuza mahusiano ya kina.

Rais huyo wa Iran amesema kuwa taarifa za uelewa tofauti katika nyanja za nishati, biashara, utamaduni, utalii na afya zitatiwa saini ingawa hata hivyo hakutoa maelezo kuhusu mikataba hiyo.