Ufaransa

Jiko la gesi lasababisha Jengo kuporomoka na kuua watu watatu nchini Ufaransa

RFI

Watu watatu wameuawa huku wengine kumi na wanne wakijeruhiwa katika mporomoko wa ghorofa moja kwenye mtaa wenye watu wengi wa mji wa Raims nchini Ufaransa.Tukio hilo limetokea jana mchana ambapo juhudi za uokozi ziliendelea huku watu wanne waliokuwemo katika ghorofa hiyo kukosekana.

Matangazo ya kibiashara

 

Mashahidi katika jiji hilo wamesema chanzo cha tukio hilo ni mlipuko uliosababishwa na jiko la gesi, uliotikisa nyumba hiyo na kuvunja vioo.

Miongoni mwa watu kumi na wanne waliojeruhiwa kuna watoto ambao hata hivyo umri wao haukutajwa, huku watu wanne wakikosekana ambapo juhudi za uokozi zinaendelea.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametuma salama za rambirambi kwa familia zilizo poteza ndugu zao.