UINGEREZA

Mchezaji wa Tottenham Gareth Bale ashinda tuzo za uchezaji bora Uingereza

RFI

Mchezaji wa Klabu ya Tottenham ya Uingereza Gareth Bale ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa chama cha soka la kulipwa, PFA.

Matangazo ya kibiashara

Aidha mchezaji huyo ametangazwa kuwa ndiye mchezaji bora wa soka kwa wachezaji wenye umri mdogo huku yeye akiwa na umri wa miaka 23.

Mchezaji huyo anakuwa wa tatu kushinda tuzo zote mbili katika msimu mmoja na yeye mwenyewe amesema hiyo ni heshima kubwa kwake.

Katika kinyang'anyiro cha kupata tuzo hizo alikabiliana na mchezaji wa Liverpool's Luis Suarez na Robin van Persie wa Manchester United.

Wachezaji ambao wamewahi kushinda tuzo hizo na Robin van Persie wa Arsenal 2011-12, Gareth Bale wa Tottenham 2010-11, Wayne Rooney wa Man Utd 2009-10, Ryan Giggs wa Man Utd 2008-09 na Cristiano Ronaldo wa Man Utd 2007-08.