Rais wa Ufaransa ayataka mataifa ya Ulaya kumaliza tatizo la ajira
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaka mataifa ya Ulaya kuhakikisha yanasimama kidete kumaliza tatizo la ajira ambalo limezikumba nchi hizo sambamba na kuangalia hatua za kuimarisha uchumi wa mataifa husika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hollande ametoa kauli hiyo alipokuwa anaongea na wanahabari akiadhimisha mwaka wake mmoja akiwa madarakani huku akitaka nchi za Ulaya kuwa na mkakati mzuri katika masuala ya bajeti za serikali na ukusanyaji wa kodi.
Kiongozi huyo ambaye amekuwa akikosilewa mno na hata wengine kueleza umashuhuri wake umeshuka katika kipindi cha mwaka mmoja amesema watahakikisha wanaimarisha bajeti ya Ufaransa kila mwaka.
Hollande aliingia madarakani mwaka mmoja uliopita baada ya kumwangusha rais wa zamani wa nchi hiyo aliyehudumu kwa muhula mmoja pekee Nicolas Sarkozy katika duru la kwanza la uchaguzi nchini humo.